Baada ya kuondoshwa katika hatua ya 16 Bora ya michuano ya AFCON
2021 kwa kuchapwa
1-0 na Gambia, wachezaji wa Timu ya taifa ya Guinea wanaocheza nje
ya taifa hilo wamepitiliza moja kwa moja kurudi katika mataifa wanayocheza soka
la kulipwa kutokea Cameroon.
Mastaa hao wameogopa kurejea na timu
hiyo nchini Guinea kama utaratibu unavyotaka kwa hofu ya kukutana na Kiongozi wa nchi Jenerali Mamady Doumbouya.
Kiongozi huyo aliyeingia madarakani kwa
mapinduzi ya kijeshi aliwaambia wazi wachezaji hao wasirejee nchini humo bila
taji hilo la AFCON 2021 wakati akiwakabidhi bendera ya nchi hiyo walipokuwa
wakielekea Cameroon.
0 Maoni