Wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria, Maduka Okoye ambaye ni golikipa na kiungo Alex Iwobi wametishiwa kuuwawa baada ya timu yao ya taifa kuondolea kwenye mashindano na Tunisia siku ya jumapili.
Kutokana na vitisho hivyo golikipa wa timu ya taifa ya Nigeria Okoye alifunga sehemu ya wafuasi wake kuweza kuacha ujumbe kwenye machapisho yake (comment), huku Iwobi ambaye alitolewa dakika ya 66 kwa kupewa kadi nyekundu nae alipokea vitisho vya kuwawa, sababu ni timu yao kufungwa kwenye michuano hiyo ya AFCON 2021.
Iwobi baada ya kupata vitisho hivyo nae aliiweka akaunti yake “archived” kwa muda ili asiweze kuona vitisho ambavyo wanaigeria walikuwa wanamtishia na kuonekana kuwa wao ndio sababu ya timu hiyo kutolewa kwenye hatua ya 16 bora.
0 Maoni