Klabu ya Manchester United Imethibitisha kuwa nyumba ya Beki
Victor Lindelof ilivamiwa wakati United ikicheza ugenini dhidi
ya Brentford na kuibuka ushindi wa mabao 3-1.
Kupitia ukurasa wa Inastagram wa mke wa Lindeloaf, Maja aliindika "kuwa watu wasiojulkana walivamia nyumba yetu (Manchester) wakati wa mechi ya
Jumatano tulifanikiwa kujifungia na hakuna aliyepata madhara"
Kufuatia kadhia hiyo meneja wa muda wa United, Ralf Rangnick amesema Mswidishi huyo hatakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya West Ham kesho ili apate nafasi ya
kuwa na familia.
“Niliongea kwa dakika 25 akanielezea kwa undani kilichotokea ameomba apate muda kupumzika na familia mimi kama baba naelewa
anachopitia hivyo nimempa ruhusa.alisema Rangnick.
Polisi katiaka jiji la Manchester bado wanaendelea na msako kuwabaini waliohusika na uhalifu huo.
0 Maoni