Kiungo wa Arsenal Granit Xhaka ameomba radhi baada ya jana
usiku kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali ya Carbao Cup dhidi
ya Liverpool ulioisha kwa Suluhu.
Xhaka alitolewa dakika ya 25 baada ya kumfanyia faulo Diego
Jota na kuifanya Arsenal kucheza pungufu
kwa dakika 65.
Napenda kuomba radhi wa watu wote nawapongeza wachezaji
wenzangu kwa kupambana na kumaliza mchezo bila kuruhu goli aameandika Xhaka
kwenye ukurasa wake wa Instagram
Timu hizo zitarudiana tena kwenye mechi yam kondo wa pili
utakaochezwa Januari 20 katika dimba la Emirates, mshindi atavaana na Chelsea kwenye
fainali.
0 Maoni