Dakika 90 za mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Polisi Tanzania umemalizika kwa wananchi kuondoka na alama tatu baada ya kushinda kwa bao 1-0 mchezo uliopigwa leo Januari 23, uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha

 


Gili pekee la Yanga limefungwa na Dickson Ambundo dakika ya 64’ baada ya mshambuliaji Fiston Mayele kuwachambua mabeki wa Polisi Tanzania.

 

Yanga imeendeleza wigo wa pointi na bingwa mtetezi Simba na sasa wameicha kwa alama 10, Wananchi wana alama 35 baada ya kucheza mechi.