KLABU ya Yanga, leo Jumapili imepanga baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union, kumtambulisha nyota wake wa kimataifa ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wao.


Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, umepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa kuanzia saa 10:00 jioni.


Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alisema mchezaji huyo walimuwinda kwa muda mrefu na usajili walioufanya hawajakosea.


Mara baada ya kumaliza mchezo na Coastal hapohapo uwanjani tutamtangaza mchezaji wetu mpya wa kimataifa ambaye tayari kila kitu kimeshakamilika, imebakia tu kumtambulisha kwa wapenzi na mashabiki wetu,” alisema Manara.