Kuelekea mchezo wa Nusu
fainali ya kwanza wa Mapinduzi Cup inayoendelea
visiwani Zanzibar kati ya Bingwa Mtetezi yanga ambao watavaana na Matajiri wa
Jiji Azam Fc, Wananchi leo itakosa huduma ya kiungo wake Abubakary Salumu Sure Boy ambaye anaugua Malaria
Pia Yanga itakosa huduma ya winga wake mpya mwenye
kasi ya Denis Nkane aliyeumia katika Mtanange dhidi ya KMKM pamoja na
Beki wa Kushoto Yasini Mustafa nae alipata majeruhi katika mchezo uliopita.
Lakini kurejea kwa Fiston
Mayele Shaban Djuma na Yanick Bangala kunaipa ahueni Yanga kwenye mchezo huo wa
Nusu Fainali utakaopigwa saa 10:15 jioni.
0 Maoni