Klabu ya Yanga leo Januari 5, imeingia mkataba wa makubaliano na Kampuni za KILINET na N-Card kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na Wanachama wa klabu hiyo ambayo inaingia katika mfumo mpya wa uendeshaji kadi hiyo itakuwa inauzwa Tsh. 29,000.
Kadi hizo zitakuwa na picha ya mwanachama/shabiki Pamoja na majina yake kamili, pia kadi hiyo itamuwezesha shabiki/mwanachama kuingia uwanjani kutazama mechi, kufanya malipo na manunuzi sehemu zote zinazotumia N-card.
“Ni kadi ya kisasa ya kidigitali ambayo itakua na
jina la Mwanachama na picha yake, sasa tunakwenda rasmi kufanya mradi huu
ufanye kazi, wale Mashabiki tunaoishabikia Timu yetu sasa twende kuiongezea
thamani timu yetu, asichati Mtu yeyote kwenye group la Yanga mpaka atume
muamala wa kuonesha amelipia ada yake ya uwanachama, hatutaki Watu ambao
hawachangii Timu yetu, ni shilingi elfu 29 tu” ameongea makamu mwenyekiti wa
kamati ya usajili Yanga, Injinia Hersi Said
0 Maoni