Mchezo wa ligi kuu ya NBC
kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga umemalizika kwa wananchi kuibuka na ushindi
wa mabao 2-0 katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.
Licha ya sehemu ya
kuchezea (pitch) kutokuwa nzuri timu
zote zilijaribu kuweka mpira chini na kujarinbu kutafuta nafasi za kufunga, Fiston
Mayele ndiye aliyefungua pazia la magoli kwa upande wa Wananchi akifunga goli
safi kwa kichwa baada ya kupokea krosi ya Djuma Shabani.
Kipindi cha dakika za lala
salama na Saido Ntibazonkiza alikwamisha
mpira wavuni akiunganisha mpira wa faridi Musa na kuachia fataki kali na kufanya
ubao kusoma 2-0.
Yanga inaendelea kusalia
kileleni mwa msimamo na alama 32 baada ya kucheza mechi 12.
0 Maoni