Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi Yanga usiku wa jana imeanza vema michuano ya mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Taifa Jang'ombe kwenye uwanja wa Aman Zanzibar.
Herieth Makambo alianza kuwainua mashabiki wa Yanga baada ya kupachika goli dakika ya 32 na kwenda mapumziko wakiwa mbele.
Kijana anayekuja kwa kasi Denis Nkane akicheza mechi yake ya kwanza akiwa na uzi wa Wananchi alifungua akaunti yake baada ya kukwamisha goli la dakika ya 52.
Ijumaa Januari 7 Yanga watajitupa dimbani kucheza na KMKM majira ya saa 10: 15
0 Maoni