Klabu ya Yanga imetumia Sh  Mil 50 kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Chrispin Ngushi aliyekuwa akiwindwa pia na Simba na kumpa mkataba wa miaka mitatu.




Ngushi mwenye mabao matatu akicheza michezo 11 ya Ligi Kuu Bara msimu huu, ni wa nne kwa Yanga
kusajiliwa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.



Wachezaji wengine waliosajiliwa na Yanga na kutambulishwa ni Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ kutoka Azam FC, Denis Nkane (Biashara United) na Aboutwalib Mshery (Mtibwa Sugar).


Yanga ipo visiwani Zanzibar ikiwa inashiriki michuano ya kombe la mapinduzi na leo wanashuka dimbani kucheza na KMKM.