Meneja Habari na
Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema kuwa, kikosi cha mnyama
kipo vyema na kimejiandaa vizuri na mchezo wa Jumapili ikiwa ni pamoja na
baadhi ya majeruhi kurejea kikosini.
Akifanya mahojiano na kitup cha redio cha Efm leo Februari 11, Ahmed amesema habari njema kwa wanasimba ni kuwa habari njema ni kurejea kwa kiungo Taddeo Lwanga kikosini na wakati ule kulikua na tetesi kwamba angeachwa lakini sio kama taarifa zilivyosambaa.
"Taddeo Lwanga amerejea kikosini, sasa ni
mzima ila suala la yeye kuingia kwenye mchezo huu hilo tunamuachia kocha lakini
pia kulikua na tetesi kwamba Simba ilitaka kumtema, naomba niweke sawa hapo
kwamba sisi tulipata ushauri wa wataalam na madaktari wa timu kwamba tumuache
mpaka atakapopona vizuri, na walitupa makadirio kuwa inaweza kuwa Mwishoni mwa
mwezi Januari na sasa amerejea tena"
0 Maoni