Bondia Amir Khan ametamba kumpiga Kell Brooks kwenye pambano maalum la kumaliza ubishi kati ya wapizani hao wa muda mrefu la SuperWelter Weight (Uzito wa kati) linalotaraji kuchezwa Jumamosi ya Februari 19, 2022 pambano litakalopigwa Manchester nchini England.

 





 Amir Khan ametamba kumpiga Kell Brooks kwenye pambano maalum la kumaliza ubishi kati ya wapizani hao wa muda mrefu la SuperWelter Weight (Uzito wa kati) linalotaraji kuchezwa Jumamosi ya Februari 17, 2022 kwenye Ulingo uliopo Manchester nchini England.


 

Khan (35) amesema “Itakuwa kitu cha kunisikitisha sana kwenye maisha yangu ya ngumi kama nikipoteza kwa Kell Brook. Hiyo ndiyo sababu ya kwenda kwenye mpambano huo nikiwa tayari kwa 100% na natakiwa kumpiga kwa namna nzuri”

 

“Kila mtu anaona hatupendani. Siwezi kupoteza kwa mtu kama Kell Brook” aloingeza Amiri Khan.

Naye Brooks (35) amejigamba kumshushia makonde na kumshinda Amir Khan kwa kupunguza uzito wake katika pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu na wafuasi wengi wa ndondi England na Ulimwenguni kiujumla.