Arsenal imefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu mbele ya Wolverhampton Wanderers baada ya kushinda kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu England, ulichezwa usiku wa jana Alhamisi kwenye uwanja wa Molineux, Wolverhampton.
Bao pekee la Gabriel Martinelli dakika ya 25, kwa
ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 39 katika mchezo wa 22 na kupanda nafasi
ya tano ikiizidi wastani wa mabao Manchester United, ambayo pia imecheza mechi
moja zaidi.
Wolves inabaki na pointi zake 34 baada ya kushuka dimbani mara 22 katika nafasi
ya nane.
Katika mchezo huo Arsenal ililazimika kucheza
pungufu baada ya Gabriel Martinelli kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 69.
0 Maoni