Arsenal wamevunja mkataba na mshambuliji wao Pierre-Emerick
Aubameyang ili aweze kujiunga na Fc Barcelona kwa uhamisho wa moja kwa moja na
sio mkopo kama ambavyo ilikuwa awali.
Dili la mkopo limekwama baada ya Arsenal kukataa kulipa
sehemu ya mshahara wa mchezaji huyo wa
kimataifa wa Gabon, paundi laki 350,000 ambazo ni zaidi ya Tsh Bil 1.8
Kuvunja mkataba kumewarahishia kazi Barca na kukabaliana
na Auba ambaye amekuwa mchezaji huru masaa matatu kabla ya dirisha la usajili
kufungwa.
Aubameyang amesaaini mkataba wa miezi sita wenye
nyengoza ya kuongeza mwaka mmoja.
0 Maoni