Staa wa kimataifa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang amethibitisha kuwa ameondoka katika klabu ya  Arsenal kwa sababu ya kutoelewana na kocha wa timu hiyo Mikael Arteta.

 




Nahodha huyo wa zamani wa Gunners leo akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa rasmi  na Barcelona ameweka wazi kuwa  uhusiano kati yake na Arteta ulianza kwenda kombo baada ya kumvua unahodha kutokana na makosa ya kinidhamu.

 

Aubameyang alitoroka kambini Dubai na kwenda Hispania kukamilisha dili hilo bila idhini ya klabu siku ya mwisho kabla ya usajili kufungwa.

 

“Nafikiri tatizo ilikuwa kwake hakuwa na furaha na mimi akamua kufanya maamuzi, kwa upande  wangu kilikuwa kipindi kigumu lakini nilitulia, huwa inatokea kiwenye mpira lakini yalishapita”

 

Akizungumzia kuhusu klabu yake mpya Auba amesema ni nafasi ambayo alikuwa akisubiria kwa hamu kubwa na pindi ilipotokea hakusita kuichukua “nilikuwa na ndoto za kucheza La liga ni nafasi adhimu kwangu kuipata  kila mmoja anajua Barcelona ni klabu bora duniani.