Ligi kuu ya NBC imeendelea jana usiku, ambapo Azam fc walikuwa wenyeji wa Dodoma jiji na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, mchezo ulipigwa uwanja wa Chamazi Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.




Mabao ya Azam Fc yamefungwa na mastraika wake wa kigeni, Mzambia Rodge Kola dakika ya 5’ na Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 64.


Kwa ushindi huo, Azam FC imezidi kuzinyemela Simba,Yanga kwenye msimamo wa ligi na sasa inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 14 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi pointi mbili Mbeya City ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.


Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 17 za mechi 14 sasa baada ya kucheza mechi 14 pia katika nafasi ya nane.

 

Ligi hiyo inaendelea leo kwa vinara wa Yanga kuwakaribisha Mbeya City mchezo utakaopigwa saa 1:00 Usiku dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam.

 

Mechi nyingine ni Kagera Sugar dhidi ya Coastal Union uwanja wa Kaitaba, na KMC dhidi Biashara United utaokaochezwa Azam Complex Chamazi.