Azam FC imeweka wazi kuwa malengo yao makubwa msimu huu ni kuhakikisha wanashinda michezo mingi kadiri inavyowezekana ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo na kukata tiketi ya kucheza mashindano ya kimataifa msimu ujao.
Azam inayonolewa na kocha Abdi Hamid Moallin, kwenye nafasi ya tatu na pointi zao 24 walizokusanya kwenye michezo 14.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ ameliambia Championi Jumamosi kuwa: “Tunajua wazi kuwa ligi ya msimu huu ni ngumu na kama klabu kila mtu anajua ni namna gani tulipitia kipindi kigumu mwanzoni mwa msimu huu, lakini kwa sasa tumerekebisha sehemu kubwa ya mapungufu tuliyokuwa nayo.
0 Maoni