Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya klabu hiyo, Morrison amekuwa na tabia ya kutoka kambini bila ruhusa kinyume na taratibu.
Mara ya mwisho mchezaji huyo alitoka kambini na uongozi wa benchi la ufundi ulimpa maelekezo kuwa asirejee kambini hapo mpaka atakapoonana na mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez imeeleza taarifa hiyo.
Aidha ametakiwa kutoa maelezo ya maandishi kwa mtendaji mkuu wa Simba ana akishindwa kufanya hivyo hatua zaidi za kinidhamu zitachukuliwa.
0 Maoni