Leo Februari 2, mtanange wa
nusu fainali ya kwanza ya michuano ya
soka ya mataifa barani Afrika AFCON inatajiwa kupigwa kati ya Burkina Faso
dhidi ya Senegal kuwania nafasi ya kutinga hatua ya fainali ambayo utachezwa
jumapili.
Timu
zote mbili hazijawahi kutwaa ubingwa wa Afrika, Senegal wamecheza fainali mbili
za michuano hii na zote wamepotea walicheza fainali ya kwanza mwaka 2002
walifungwa kwa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Cameroon na mwaka 2019 walifungwa
bao 1-0 na Algeria.
Burkina Faso
ambao pia ni washindi wa 3 wa fainali zilizopita za mwaka 2019 wanaiwinda
fainali ya pili baada ya kucheza fainali yao ya kwanza kwenye michuano hii
mwaka 2013 fainali ambayo walipoteza kwa kufungwa bao 1- 0 na timu ya
taifa ya Nigeria.
Je
nani ataibuka mbabe kwenye mchezo huu wa kutafuta nafasi ya kuingia Fainali majibu
ni saa leo 10:00 usiku.
0 Maoni