Wenyeji wa michuano ya Afcon jana usiku  kushinda nafasi ya mshindi wa tatu kwa kuibuka na ushindi kwa penati 5-3 baada ya kutoka sara ya 3-3 dhidi ya Burkina Faso mchezo uliopigwa uwanja wa Ahmadou-Ahidjo in Yaounde, Cameroon.

 




Burkina Faso walianza vema kwa mchezo huo kwani mpaka dakika ya 50’  walikuwa mbele kwa mabao 3-0 mabao yakifungwa na Steeve Yago dakika ya 24, bao la kujifunga la kipa wa Cameroom André Onana  dakika ya 43, na Djibril Outtara dakika ya 49.

 

Cameroon waligeuza kibao na kuanza kusawazisha kuptia kwa Bahokem na magoli mawili ya haraka haraja ya kinara wa mabao kwenye michuano ya mwaka huu nahodha wa Vincent Aboubakar na kulazimisha mchezo kuongezea dakika 30 ili kumpata mshindi.

 




Dakika hizo zilimalizika hakuna mbabe ndipo  mikwaju ya penati ikaamua mchezo huo na Cameroon kuibuka kidedea kwa kushinda penati 5-3 kutwaa nafasi ya mshindi wa tatu.


Mchezo wa Fainali ya michuano hiyo unachezwa leo kati ya miamba ya Afrika Magharibi Senegal ambao wataongozwa na mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane dhidi ya Misri ambayo itaingozwa na mchezaji wa Liverpool Mohamed Salah.