Klabu ya Manchester City ya England imethibitisha kumuongezea mkataba wa miaka miwili  beki Mreno Joao Cancelo, utakaomfanya kuwepo Etihad hadi mwaka 2027.



Mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika 2025 lakini City walikuwa na nia ya kumpa mchezaji huyo mkataba ulioboreshwa zaidi kama zawadi kutokana na ubora wake, anaonyesha uwanjani.

 Cancelo ameng’ara pande zote za safu ya ulinzi ya City, akipachika mabao matatu na kutoa pasi 8 za mabao (assist) msimu huu.

“Manchester City ni klabu kubwa, nina furaha kubwa kusaini mkataba huu mpya,” alisema baada ya kusaini dili hilo nono.