Goli kipa wa Manchester United David de Gea, amechaguliwa kuwa mchezaji bora ligi kuu ya England wa mwezi Januari hii ikiwa ni mara ya kwanza kubeba tuzo hiyo tangu ajiunge na United mwaka 2011.

 




Mhisipania huyo (31) ameokoa michomo ya hatari 22 katika michezo minne ya ligi na kuisadia Man United kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Epl.

 

De Gea amewashinda wachezaji wengine sita ikiwa ni Pamoja na Jarrod Bowen, Kevin De Bruyne, Jack Harrison, Joao Moutinho na James Ward-Prowse.


mara ya mwisho kwa kipa kushinda tuzo hiyo ilikuwa mwaka 2016 ikienda kwa aliyekuwa mlinda mlango wa Southampton Fraser Forster