Staa wa
tennis Mserbia Novak Djokovic amesema yupo tayari kukosa michuano mikubwa ijayo
ya tennis (French open na Wimbledon open) kama itakuwa lazima kuchanja kama ilivyokuwa
kwenye michuano ya wazi ya Australian 2022 yaliyomalizika mjini Melbourne mwezi
Januari 31.
"sijawahi kupinga
chanjo hata siku moja kwa sababu nilipokuwa mdogo nilipata chanjo kadhaa, lakini
kila siku naunga mkono uhuru wa mtu kujiamulia kitu gani kiingine kwenye mwili
wake na nipo tayari kulipa gharama ya kutoshiriki kwenye mashindano yajayo kisa
kubaki na msimamo wangu wa kutochanjwa "amesema Djokovic
Djokovic mwenye umri wa
miaka 34, anayeshuka nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango wa tenisi duniani
kwa upande wa wanaume akiwa mataji makubwa 20 ya tennis (Grand Slams)
alizuiliwa kushiriki kwenye michuano ya wazi ya Australian mwaka 2022 baada ya
kuzuiliwa kutokana na kutochanjwa chanjo ya Uviko 19 na kunyang'anywa pasi yake
ya kusafiria ya kuingia nchini humo.
0 Maoni