Baada ya kupitia kipindi kigumu cha kuandamwa na majeraha, hatimaye mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube, amesema
kuwa kwa sasa yupo fiti, anataka
kupambana na kuifungia mabao
mengi timu yake.
Dube
amesema msimu uliopita alipishana
na kiatu cha ufungaji bora kwa
sababu alikuwa anaumia mara kwa
mara, lakini kwa sasa yupo fiti na
anarudi akiwa na nguvu kubwa uwanjani.
Akizungumzia
hali yake kiafya na mwenendo
wa ligi tangu kuanza kwa msimu
huu, Dube alisema kumekuwa na
mabadiliko makubwa kwa timu nyingi
na ushindani umeongezeka, ila
kwa kuwa amepona na kuwa fiti,
atafanya kile mashabiki wake wanataka.
“Msimu
niliuanza vibaya kutokana na
majeraha niliumia sana kwa sababu malengo
yalikuwa ni kuisaidia timu ila nashukuru nimerejea na
nipo tayari kwa
hilo,” alisema.
0 Maoni