Klabu ya Everton ya England imekamilisha usajili wa
Dele Alli, kutoka Tottenham Hotspurs dakika chache kabla ya kufungwa kwa dirisha
dogo la usajili jana saa sita usiku, kwa dau la paundi mil.40 kwa mkataba wa miaka miwli na nusu.
Delle ambaye ameichezea Spurs mechi 269 na kufunga
magoli 67 tangu alipojiunga na timu 2015, anaungana na kocha mpya Frank Lampard
pamoja na Donny van de Beek alijiunga kwa mkopo hadi mwisho wa msimu akitokea
Mancheter United.
Huenda mchezaji huyo wa kimataifa wa England akawa
sehemu ya mchezo wa ligi kuu England dhidi ya Newcastle United Jumanne ijayo.
0 Maoni