Uongozi wa Kampuni ya GSM leo Februari 7, 2022,umetangaza rasmi kujiondoa kwenye nafasi ya kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu ya NBC [NBC PREMIER LEAGUE].
Sababu kubwa iliyofanya GSM kufikia maamuzi hayo ni kwa TFF pamoja na Bodi ya Ligi Kuu kushindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vya kimkataba kama pande hizo mbili zilivyokubaliana, pia mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya Taifa Stars, Ghalib Said Mohamed amejiuzulu nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Allan Chonjo, Afisa Biashara Mkuu GSM, amesema GSM ilishawishika sana na TFF pamoja na Bodi ya Ligi na kuridhia kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu ili kukuza sekta ya Mpira wa Miguu hapa nchini pamoja na michezo kwa ujumla lakini hili halikuenda kama lilivyokusudiwa.
Chonjo amesema, hayajawa maamuzi rahisi kwa kampuni ya GSM kwani wanatambua ya kuwa vipo baadhi ya vilabu vya mpira vitakavyoumizwa pamoja na wadau mbalimbali na hatua hii na wala haikuwa dhamira yao kufikia uamuzi huo mgumu.

0 Maoni