KLABU ya Yanga leo Februari 18 imefanya uzinduzi wa kadi mpya za Uanachama za kieletroniki kwa Wabunge wa Bunge Ia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wanachama wa Yanga.
Uzinduzi wa kadi za kielektroniki ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko ya kidigitali na ya mfumo wa uendeshaji wa klabu kwa mujibu wa katiba ya Yanga toleo Ia 2021.
Hafla ya uzinduzi huo umefanyika kwenye Hoteli ya Morena jijini Dodoma kuanzia saa 4:00 asubuhi ambapo mgeni rasmi alikuwa Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Wabunge, Viongozi wa Klabu ya Yanga, wadau na waandishi wa habari.
0 Maoni