BEKI kiraka wa Yanga, Kibwana Shomari na mwenzake Abdallah Shaibu ‘Ninja’,wanahesabu siku tu za kurudi uwanjani mara baada ya kupona majeraha yao.




Kibwana anayemudu 
kucheza beki wa kulia na kushoto, wiki mbili zilizopita alikwenda Tunisia sambamba na Ninja kwa ajili ya kufanyiwa operesheni ya majeraha yanayowasumbua.



Kurejea kwa mabeki hao 
kutampa upana wa kikosi Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.



Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra na kuthibitishwa na daktari wa timu hiyo, Youssef Ammar, mabeki hao watarejea uwanjani mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Februari 5, mwaka huu.