Nyota  wa soka anayekipiga West Ham Kurt Zouma (27) amepoteza dili lake la udhamini na kampuni ya Adidas baada ya kuonekana kwa video akipiga paka , ambapo video  imesambaa kwenye mitandao mbalimbali.



Taarifa ya Adidas imesema “Tumehitimisha uchunguzi wetu na kuthibitisha kuwa Kurt Zouma sio mwanamichezo wa Adidas tena”


Hata hivyo timu yake ya West Ham imempiga faini ya pound 250,000 (Tsh milioni 783) kwa kosa hilo alilofanya la kuwapiga paka na kusema pesa hizo zitapelekwa kwenye Taasisi zinazosimamia Wanyama