Kocha msaidizi wa Misri Diaa al-Sayed ameomba fainali yao ya
Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Senegal ichezwe Jumatatu badala ya Jumapili
ili wapate siku ya ziada ya kupumzika.
Mafarao waliwashinda
wenyeji Cameroon siku ya Alhamisi kwa mikwaju ya penalti, ukiwa ni ushindi wao
wa tatu mfululizo.
Senegal, ambao
wameshinda michezo zao zote ndani ya dakika 90, walishinda Burkina Faso 3-1
Jumatano.
"Naomba CAF
fainali ichezwe Jumatatu," Senegal wana siku moja ya ziada ya kupumzika'' alisema
Al-Sayed.
Al-Sayed alikuwa akizungumza na vyombo vya habari kwa sababu
kocha wa Misri Carlos Queiroz alitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati wa mechi.
Mechi ya kutafuta
mshindi wa nafasi ya tatu kati ya Cameroon na Burkina Faso ilipaswa kuwa
Jumapili pia, lakini sasa itachezwa Jumamosi tarehe ya fainali na endapo itasogezwa
itachelewesha wachezaji kurejea kwenye vilabu vyao.
Credit: BBC
0 Maoni