Majogoo wa jiji Liverpool
wameendelea kuifukuzia Manchester City kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Leicester City mchezo wa ligi kuu England uliochezwa Alhamisi usiku uwanja wa Anfileld.
Magoli ya Mreno, Diogo Jota dakika ya 34 na 87 na kufikisha
pointi 51 baada kucheza mechi 23, ikiwa katika nafasi ya pili, ikizidiwa pointi
tisa na mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Leicester City inabaki kwenye nafasi ya 12 na
pointi zake 26 baada ya mechi 21.
0 Maoni