Mabigwa wa Ulaya Chelsea wametinga hatua ya Fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Dunia baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa wa Bara la Asia Al-Hilal mchezo uliopigwa Abu Dhabi Falme za Kiarabu.
Goli pekee la The Blues limefungwa na Romelu Lukaku dakika ya 32, Chelsea
sasa itavaana na mabingwa wa Brazil na bara la Amerika ya Kusini Palmeiras siku
ya Jumamosi Februari 12.
Chelsea inasaka rekodi ya kuwa timu ya tatu kutoka England
kutwaa kombe hilo, timu zilitwaa kuombe hilo ni Manchester United na Liverpool.
0 Maoni