Manchester United imeendelea kususua kwenye ligi kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Burnely, mchezo uliopigwa usiku wa jana.
Paul Pobga alifunga bao lake la kwanza tangu Januari 2021 na kuipa uongozi United, lakini Jay Rodriguez alikata matumaini ya United kuondoka alama tatu baada ya kuisawazia Burnely dakika ya 47.
Kwa matokeo hayo Man United imeshuka kwa nafasi moja kwenye msimamo wa Epol, kutoka ya nne hadi ya tano ikiwa na alama 39.
0 Maoni