Manchester United ikiwa katika uwanja wa nyumbani Old Trafford imetolewa nje ya kombe la Fa jana usiku na timu ya Middlesbrough kwa penati 8-7 baada ya dakika  90  na nyongeza 30 kumalizika kwa sare ya 1-1.

 


Ilikuwa siku mbaya kwa staa wa United Cristiano Ronaldo baada ya kukosa penati ambayo ingeipa uongozi, hii ikiwa ni penati ya nne kwa Ronaldo kukosa tangu aichezee  Man United.

 

Jadon Sancho alifunga goli la kuongoza dakika ya 25 goli ambalo lilidumu hadi kipundi cha kwanza kinaisha, lakini kiungo wa Middlesbrough Matt Crooks alisawazisha kwa goli la utata, baada ya kunawa mpira kabla ya kufunga, lakini VAR ikaruhusu goli hilo.

 


Katika mikwaju ya penati kinda Anthony Elanga alikosa mkwaju wa penati na kuifanya Man United kutupwa nje ya michiano hiyo.