Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya ligi Kuu Tanzania TBLP katika kikao chake cha Februari 10, 2022 ulipitia mwenendo na matukio mbalimbali ambapo imewatoza faini ya 500,000 kila Maofisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli na Haji Manara kwa kosa la kuwashutumu Waamuzi wa Ligi  kuu ya NBC kupitia vyombo vya habari.



Bumbuli na Manara walizungumza na wanahabari Februari 8, 2022 kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu huyo ambapo waliwashutumu waamuzi wa ligi kuu kwa masuala mbalimbali walioyahusidha na upendeleo.