Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema wachezaji wa Klabu hiyo walilazimika kumeza Panadol sita sita kabla ya kucheza mchezo wao wa Ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Sumbawanga mkoani Rukwa.
Akizungumza na wanahabari leo Februari 8, 2022 amesema walifuata taratibu zote za kuomba mchezo huo usogezwe mbele kutokana na wachezaji wengi kuwa wagonjwa lakini walishindwa kwa kuambiwa kuwa walikosea kufuata taratibu.
Manara amesema alishangaa kuona Klabu ya Simba ilikubaliwa ombi lao la kusogezwa mbele mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar kukubaliwa huku wao wakinyimwa ruhusa hiyo.
"Hakuna mechi ngumu msimu huu kama ile tumecheza na Prisons, wamecheza kina Mwamnyeto na Mapanadol sita sita ila tukawaambia nyie ni wanaume pambaneni" amesema Manara
"We umewahi kuskia mchezaji Half time anakula Panadol? Yes siwatanii na tulipambana"
Kwanini ruhusa ya kuahirisha mchezo, ilipata Simba pekee huku klabu ya Yanga ikinyimwa fursa hiyo? amehoji Manara
0 Maoni