Manchester City imeendeleza ubabe kwenye ligi kuu ya England
baada ya kuichapa Brentford kwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa jana usiku kwenye
uwanja wa Etihad, Manchester.
City walipata magoli yao kupitia kwa mchezaji wa kimataifa
wa Algeria Riyad Mahrez kwa mkwaju wa penati baada ya Rahim Sterling kuchezewa
faulo ndani ya 18.
Vijana wa Pep Guardiola waliongezaa bao la pili na kujihakikishia
alama tatu kupitia Kevin de Bruyne, city wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama
kwa tofauti ya pointi 12, wakiongoza kwa alama 60 wakiwaacha Liverpool kwenye
nafasi ya pili na alama 48.
Matokeo ya michezo mingine ya Epl iliyochezwa jana ni kama ifuatavyo👇👇👇
0 Maoni