Senegal
imetinga hatua ya fainali ya michuano ya Afcon bada ya kuishushia kipigo timu
ya taifa ya Burkina Faso cha mbao 3-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa jana
usiku katika dimba la Ahmadou Ahidjo, Yaounde
Cameroon.
Abdou Diallo alianza kufungua akaunti ya mabao baada ya kuiandikia Senegal bao la kuongoza dakika ya 70,dakika sita baadaye Idrissa Guaye anayekipiga PSG ya Ufaransa, akakwamwisha mpira wavuni akimalizia pasi safi ya Sadio Mane nakuandika bao la pili kwa Senegal.
Burkina Faso
wakaamka na kufanikiwa kupata bao dakika ya 82 kupitia kwa Blati Toure na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Nyota wa Liverpool Mane ndiye aliyezima ndoto za
Burkina Faso za kwenda fainali baada ya kuweka kimiani bao la tatu kunako
dakika ya 87 ya mchezo.
Hii ni fainali ya tatu kwa Senegal wakiwafanya hivyo mwaka
2002, 2019 ambazo zote walipoteza, mshindi wa mechi ya leo kati ya mwenyeji
Cameroon dhidi ya Misri atacheza na Simba wa Terenga kwenye mchezo wa
fainali jumapili.
0 Maoni