Shirikisho la soka Afrika CAF limeruhusu mashabiki 35,000 kuhudhuria mchezo
wa kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Simba dhidi ya ASEC Mimosas mchezo
ukataochezwa jumapili Februari 13,
kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.
Akitoa taarifa hiyo leo Februari 1, meneja wa Habari na Mawasilino wa klabu
hiyo Ahmed Ally amesema waliomba kupatiwa idadi kubwa zaidi ya mashabiki lakini
mamlaka husika wamruhusu idadi hiyo ya mashabiki.
Aidha mashabiki wamekubushwa kuchukua tahadhari zote za Covid 19, ikiwemo kutakasa mikono kuvaa barokoa, kukaa kwa nafasi kwa mashabiki watakaingia uwanjani (social distance) na siku ya mchezo tiketi hazitauzwa uwanjani.
0 Maoni