Katika kuhakikisha wachezaji wake wanaepukana na majeraha ya mara kwa mara, daktari wa viungo wa Yanga.



Mtunisia Youssef Ammar amewapiga stop mastaa wa timu hiyo kutumia vyakula aina ya Burger na Pizza.



Hiyo ni katika kuhakikisha wanapunguza 
ongezeko la wachezaji wenye majeraha katika kikosi chao hicho ambacho kimepiga kambi huko Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.




Daktari huyo hivi sasa anawapambania 
nyota wake watatu warejee uwanjani ambao aliwapeleka nchini Tunisia kwa ajili yakufanyiwa upasuaji hivi karibuni kutokana na kuwa matatizo ya goti.


 

Wachezaji hao waliofanyiwa upasuaji ni Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Mburkinabe, Yacouba Songne.



kwa Mujibu wa Championi Jumatano, Ammar alisema kuwa vyakula vya aina hiyo ya Burger na Pizza chanzo cha wachezaji kupata majeraha yasiyotegemewa katika timu.


Chanzo-Gazeti la  Championi