Lionel Messi mshindi mara saba wa wa tuzo za Ballon d’Or inawezekana akawa anapitia kipindi kigumu katika maisha yake ya soka baada ya kuandamwa na ukame wa mabao akiwa na timu mpya ya Paris Saint Germain aliyojiunga nayo akitokea Fc Barcelona.




 

Juzi Jumapili Lionel Messi amefanikiwa kufunga bao lake la pili ndani ya Ligue 1 baada ya kupita dakika 477.


 

Messi alifunga bao lake hilo la pili wakati PSG ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Lille Katika mchezo huo, Messi alifunga bao moja na kutoa asisti moja .


 

Messi tangu atue Ligue 1 msimu huu wa 2021-22, bao lake la kwanza alifunga Novemba 20, 2021 wakati PSG ikivaana na Nantes na waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo huo ambao alicheza kwa dakika 90.



Mpaka sasa ndani ya Ligue 1 kwa ujumla amehusika katika mabao tisa akifunga mabao mawili na asisti saba akicheza jumla ya dakika 982 sawa na mechi 13 za ligi hiyo kwa msimu huu mpaka sasa.