Rais
wa heshima wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ Februari 9, amekutana na kuzungumza na
wachezaji na benchi la ufundi la tomu hiyo kuelekea mchezo
wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosa ya Ivory Coast.
Akizungumza
Azam Tv mara baada ya kikao hicho Dewji amesema malengo makuu ni
kufanya vizuri kwenye michuano hiyo baada ya kutolewa kwenye ligi ya mabingwa.
“Tunahitaji
ubingwa na mafanikio ya kimataifa, maana hata mimi licha ya kupata hasara
katika uendeshaji wa klabu bado naendelea kutoa fedha na ninyi nataka
mkajitume”
Mashabiki
wa Simba ni wa muhimu sana kwa maendeleo ya klabu yetu, natangaza kupunguza
viingilio na Jumapili mzunguko itakuwa elfu 3 ili wote waweze kuitazama timu
yao" Mo Dewji.
Simba
itawavaa ASEC Mimosas ya Ivory Coast Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa
Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
0 Maoni