Taarifa kutoka Gazeti la MwanaSpoti ni kwamba, Bernard Morrison amepewa ofa ya usajili wa Tsh. Milioni 230 na Mshahara wa Milioni 18 kwa mwezi ili aweze kujiunga na Yanga Sc.
Mkataba wa Morrison ndani ya Simba umesaliwa muda usiozidi miezi mitatu na mabosi wa klabu hiyo wamemsimamisha kwa kudaiwa kutoroka kambini kwa kuruka ukuta, pamoja na kufanya vituko vingine kambini.
Lakini, habari za uhakika zinasema Mghana huyo aliyeondoka kwa kuwakera wanayanga anarejea tena kunako klabu hiyo iliyomleta nchini, baada ya matajiri wa klabu hiyo kumwekea mzigo wa maana ili kunasa saini yake.
0 Maoni