Baada ya mwaka jana kuweka wazi kuwa amefanya upasuaji (sajari) za dimpozi na umbile kwa ujumla, mwanamama Muna Love amejitokeza na kuwasihi watu kutofanya sajari kwani anajuta na kuahidi kuweka wazi madhara yake hivi karibuni.





Muna Love ambaye anadaiwa kulazwa hospitalini kutokana na madhara ya sajari ameandika ujumbe huu kupitia Insta Story yake; “Achaneni na surgery. msifanye nitakuja kuwaeleza vitu vingi ninavyopitia. Nampenda Yesu, nawapenda…”