Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya ligi Kuu Tanzania TBLP katika kikao chake cha Februari 10, 2022 ulipitia mwenendo na matukio mbalimbali kwenye ligi hiyo 
 

Kamati hiyo imemtoa  kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko  mitatu Mwamuzi Ahmada Simba aliyechezesha mchezo kati ya Simba dhidi ya  Tanzania Prisons  katika uwanja wa Benjamin Mkapa Februari 3 2022 kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpirawa miguu kwenye mchezo huo. 


Mechi hiyo  iliisha kwa Simba kupata ushindi wa goli 1-0 kwa Penati iliyopigwa na Meddie Kagere.