Mkongwe kunako Bongo Fleva  ambaye ni Mbunge wa jimbo la Muheza  Tanga, Hamis Mwinjuma maarufu Mwanafalsa (Mwana Fa) ametimiza miaka 20 kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Flava.


Mwana Fa  kupitia jukurasa wake wa Instagram ameandika; “Wimbo wangu wa kwanza INGEKUWA VIPI? ulitoka siku yenye tarehe kama ya leo (02/02) mwaka 2002. the rest is history...


“Namshukuru Mungu kwa kunipa miaka 20 na bado inahesabu kwenye hii kitu fam! na wote mlioniunga mkono kwenye hii safari.


“Wakati tunaadhimisha nisaidie kunitajia wimbo wako bora toka kwangu, nataka kujua tu kama tukifikiria kutoa wimbo mwingine uelekee wapi…”