KOCHA Mkuu wa vinara wa Ligi kuu ya NBC, Yanga, Nasreddine Nabi, ameweka wazi kuwa anaamini kama kikosi.chake kitaendelea na kasi ambayo wanaenda nayo kwa sasa, basi ni wazi hakuna timu inayoweza kuwazuia katika malengo yao ya kushinda ubingwa wa ligi kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).




Yanga  Jumamosi 
wakiwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, walifanikiwa
kushinda 1-0 dhidi ya 
Mbao katika mchezo wa hatua ya 32 ya ASFC, ushindi huo umewafanya wakate tiketi ya kucheza hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.




 

Tayari msimu huu Yanga wamefanikiwa kushinda taji la Ngao ya Jamii na mpaka sasa wao ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu bara na poiti zao 35, walizokusanya kwenye michezo 13.