Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemtangaza muamuzi Victor Gomes Raia wa Afrika Kusini kuwa ndio atakayechezesha mchezo wa fainali kati ya Senegal dhidi ya Misri kesho nchini Cameroon.
Mwamuzi huyo amekuwa akichezesha michezo ya ligi kuu ya Afrika ya kusini tangu mwaka 2008 alipata beji ya FIFA mwaka 2011 na tayari amechezesha michuano mbalimbali mikubwa duniani kama vile, AFCON 2015, 2019 na hii ya mwaka huu ambayo amepewa rungu la kusimamia sheria 17 dimbani.
Kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka
17 iliyofanyika nchini Brazil mwaka 2019 michuano ya Olimpiki iliyofanyika mwaka 2021.
Victor Gomes raia wa Afrika Kusini ndiye amepewa
dhamana ya kusimamia sheria 17 za mchezo wa soka kwenye mchezo wa fainali ya
Kombe la mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Misri siku ya Jumapili nchini
Cameroon.
0 Maoni