Baada ya Timu taifa ya Senegal kutwaa ubungwa wa AFCIB Rais wa nchi huyo, Macky Sall ametangaza leo Jumatatu kuwa siku ya mapumziko ili kusherehekea ushindi wa timu ya taifa wa Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON.


Rais Sally  ametangaza mapumziko hayo ikiwa sehemu ya  kuwakaribisha nyota hao wa soka kurejea nchini humo yaani leo Februari 7. aidha amefuta safari yake nje ya nchi ili awakaribishe mabingwa hao ikulu. 




Senegal siku ya jana wameibuka kuwa mabingwa wa baada ya kuichapa Misri kwa mikwaju ya penati na kuifanya Senegal kuchukua Kombe la Afcon kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwakwe..